MKUU WA MKOA wa Manyara JOEL BENDERA ametoa miezi Minne kwa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Watendaji wa Halmashauri kuhakikisha wanasimamia ujenzi wa Maabara katika shule za Sekondary.
BENDERA ametoa agizo hilo alipofanya ziara ya siku moja kukagua Ujenzi wa Maabara katika Wilaya za Simanjiro na Kiteto na kuzungumza na Wenyeviti wa Vijiji,Madiwani na Watumishi wa Wilaya hizo.