MKUU wa wilaya ya Masasi mkoani Mtwara FARIDA MGOMI, ametoa onyo kwa viongozi wa vijiji vya Mwongozo, Mdenga na Nangoo vilivyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Masasi, ambao wanashindwa kuwachukulia hatua za kisheria watu ambao wanahujumu miundombinu katika mradi wa maji wa mamlaka ya maji safi na Mazingira Masasi-Nachingwea -MANAWASA.
MGOMI ametoa onyo hilo baada ya Mamlaka hiyo kutangaza kusudio la kusitisha huduma ya Maji kwenye Vijiji hivyo vitatu kutokana na wananchi wake kuhujumu Miundombinu ya maji na kusababisha huduma hiyo muhimu kuzorota.