MKWASA AISIFU STARS KWAKUPAMBANA

MKWASA AISIFU STARS KWAKUPAMBANA

Like
186
0
Monday, 06 July 2015
Slider

Charles Boniface Mkwasa ‘Master’ amesema timu yake imepigana kufa na kupona na kucheza vizuri licha ya kutolewa na wenyeji Uganda (The Cranes) katika kinyang’anyiro cha kugombea tiketi ya kufuzu kucheza fainali za CHAN mwakani nchini Rwanda.

Stars imetoka sare ya bao 1- 1 dhidi ya wenyeji Uganda (The Cranes) katika mchezo wa marudiano kuwania kufuzu kwa fainali za CHAN mwaka 2017 nchini Rwanda uliofanyika uwanja wa Nakivubo Jumamosi.

Stars ilicheza soka la kuvutia tangu mwanzo mpaka mwisho wa mchezo hali iliyowaduwaza wenyeji Uganda.Mpaka dakika 45 za mchezo za kipindi cha kwanza zinamalizika, Uganda 0 – 0 Tanzania.

Kipindi cha pili kilianza kwa Stars kufanya mashambulizi mfululizo kupitia kwa washambuliaji wake John bocco na Rashid Mandawa.Dakika ya 58, John Bocco aliipatia Tanznaia bao la kwanza kwa mkwaju wa penati kufuatia mlinzi wa Uganda Bakaki Shafik kuunawa mpira wa ndani ya eneo la hatari.

Mara baada ya bao hilo Uganda walifanya mashambulizi mfululizo langoni mwa Stars na kufanikiwa kupata bao la kusawzisha dakika ya 82, kupitia kwa mchezaji Kizito Hezron.

Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika Uganda 1 – 1 Tanzania. Kwa matokeo hayo Uganda wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 4 – 1 na sasa watakutana na Sudan.Kocha wa Uganda Sredojevic Milutin ‘Micho’ amewasifu wachezaji wake kwa kuweza kuzuia mashambulizi ya Stars.

Vikosi vya timu hizo vilikuwa kama ifuatavyo:

Taifa Stars: Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Haji Mngwali, Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Mudathir Yahya, Deus Kaseke, Frank Domayo,/Said Ndemla John Bocco, Rashid Mandawa/Salum Telela, Saimon Msuva/Ramadhan Singano.

The Cranes: James Alitho, Muzamiru Mutyaba, Brian Ochwo, Hassan Waswa, Denis Oola, Faruk Miya, John Shemazi/Robert Sentongo, Bakaki Shafik, Tekkwo Derick/Kizito Hezron/Kalanda Frank.

Comments are closed.