MLONGE YAINGIA KATIKA USHINDANI NCHINI

MLONGE YAINGIA KATIKA USHINDANI NCHINI

Like
791
0
Tuesday, 18 November 2014
Local News

Tanzania imekuwa kwa kiwango kikubwa katika usindikaji na utengenezaji wa bidhaa za Mlonge hali iliyochangia soko la bidhaa hizo kuwa katika ushindani wa kibiashara.

EILEEN KASUBI ni mkurugenzi wa kampuni ya MOKAI MORINGA MLONGE amesema bidhaa za mlonge zimekuwa zikiuzika zaidi katika masoko ya ndani na nje kutokana na kuwepo kwa wajasiriamali wengi wanaosindika mlonge ingawa watanzania wengi wahajapata elimu juu ya matumizi ya bidhaa hizo.

 Amesema wajasiriamali wanaotengeneza bidhaa za mlonge wanategemea zaidi masoko ya maduka makubwa na kusema kuwa changamoto kubwa iliyopo kwao ni elimu kwa baadhi ya wajasiriamali pamoja na kutokuwa na mashirikiano.

Akizungumzia zaidi kuhusu bidhaa hizo Kasubi amesema moja ya bidhaa zinazotengenezwa na mlonge ni sabuni za majumbani ambazo zinaubora wa kimataifa na kuwataka wananchi kutumia bidhaa hizo ili kukuza soko la biashara la ndani.

KASUBI.

Comments are closed.