MMAREKANI AHUKUMIWA KIFUNGO NA KAZI NGUMU KOREA

MMAREKANI AHUKUMIWA KIFUNGO NA KAZI NGUMU KOREA

Like
273
0
Friday, 29 April 2016
Global News

RAIA wa Marekani amefungwa jela miaka 10 na kazi ngumu nchini Korea Kaskazini baada ya kupatikana na makosa ya kufanya ujasusi, shirika la habari la Uchina la Xinhua limeripoti.

Kim Dong-chul, raia wa Marekani aliyezaliwa Korea Kusini, alikamatwa mwezi Oktoba mwaka jana.

 

Kim alifikishwa kwa wanahabari mjini Pyongyang mwezi jana na akaoneshwa akikiri makosa, na kusema kwamba alilipwa na Korea Kusini kufanya ujasusi huo.

Comments are closed.