MOSES MACHALI KUJIUNGA NA ACT LEO

MOSES MACHALI KUJIUNGA NA ACT LEO

Like
257
0
Tuesday, 21 July 2015
Local News

KIONGOZI wa chama cha –ACT-Wazalendo Zitto Kabwe leo anampokea Mbunge wa Kasulu, mjini Moses Machali kutoka chama cha –NCCR-Mageuzi ambaye atajiunga na kutatambulishwa rasmi kuwa mwanachama wa –ACT-Wazalendo.

 

Machali anaambatana na Madiwani wawili, Kamishna wa mkoa mmoja na katibu wake pamoja na wenyeviti na makatibu wa kata 12 zilizo katika jimbo la Kasulu mjini., Pia katika mapokezi hayo kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe atawapokea makatibu uenezi 9 wa jimbo hilo lenye jumla ya kata 15 za uchaguzi.

 

Mbali na viongozi hao wengine watakaoambatana na Machali kujiunga na Chama cha –ACT-Wazalendo ni pamoja na wenyeviti wa matawi 101 na makatibu 98, watakaoambatana na wanachama wa awali 648 wote hao wanatoka katika Chama cha –NCCR-Mageuzi jimbo la Kasulu mjini.

Comments are closed.