MOURINHO AKATAA KAZI SYRIA

MOURINHO AKATAA KAZI SYRIA

Like
340
0
Monday, 11 April 2016
Slider

Aliyekuwa meneja wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho amekataa ombi la kumtaka awe meneja wa timu ya taifa ya Syria, wakala wake amesema.

Kupitia barua pepe iliyotumwa kwa shirika la habari la

Associated Press, Jorge Mendes amesema Mourinho aliambia Shirikisho la Soka la Syria kwamba “ameshukuru sana kupokea mwaliko, lakini hawezi akaukubali kwa sasa”.

Mreno huyo mwenye umri wa miaka 53 alifutwa kazi na Chelsea kwa mara ya pili Desemba.

Mourinho, ambaye amewahi kuwa meneja Porto, Real Madrid na Inter Milan, amehusishwa na kuhamia Manchester United.

Ripoti wiki iliyopita zilisema Mourinho ameanza kutafuta nyumba eneo la Cheshire baada ya wawakilishi wake kufanya mazungumzo na United.

Syria, ambao hawajawahi kufuzu kwa Kombe la Dunia, walimfuta kocha wao Fajr Ibrahim licha ya kufika raundi ya tatu na ya mwisho ya kufuzu kwa Kombe la Dunia barani Asia. Michuano ya raundi hiyo itaanza Agosti.

Syria wameorodheshwa nambari 123 kwenye orodha ya Fifa.

Wamekuwa wakichezea mechi zao za nyumbani Oman kutokana na vita nchini mwao.

Comments are closed.