MOURINHO: HATUJAMMISS PETR CECH

MOURINHO: HATUJAMMISS PETR CECH

Like
236
0
Monday, 10 August 2015
Slider

Kocha mbwatukaji Jose Mourinho amesema Chelsea haijammis aliyewahi kuwa mlinda mlango bora kabisa katika klabu hiyo Petr Cech na kuongeza kuwa ana uhakika mabingwa hao watetezi wataikabili vizuri kabisa klabu ya Manchester City siku ya jumapili watakaposhuka dimbani.

Mourinho hakuwa tayari kumuacha mlinda mlango huyu mwenye miaka 33, ajiunge na wapinzani wao wa London klabu ya Arsenal baada misimu 11 ya mafanikio na ubingwa .

“hatujammis Petr, alikaliliwa Mounrinho akizungumza na vyombo vya habari nchini Uingereza “tuna walinda mlango wazuri kabisa, Petr sio tatizo kwetu bali tatizo ni upinzani kuwa bora kuliko msimu uliopita.”

 

Chelsea ilifanya maamuzi ya kumnunua mlinda mlango Asmir Begovic kutoka Stoke City ili kuongeza nguvu na Thibaut kufuatia kuondoka kwa mlinda mlango mahiri Petr Cech.

Comments are closed.