MOURINHO: NAHESHIMU MAAMUZI  YA CECH PIA NATAMBUA MCHANGO WAKE

MOURINHO: NAHESHIMU MAAMUZI YA CECH PIA NATAMBUA MCHANGO WAKE

Like
171
0
Friday, 03 July 2015
Slider

Mlinda mlango kutoka jamhuri ya Czech, Petr Cech’s ambae uhamisho wake umekamilika kutoka kwa mabingwa wa ligi ya Uingereza Chelsea kwenda kukipiga katika klabu ya Arsenal uhamisho wake umeungwa mkono na meneja wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho.

Cech amekuwa chaguo la kwanza kwenye kikosi cha klabu ya Chelsea katika kipindi cha miaka 10 na baadae kuipoteza nafasi hiyo kwa mbeligiji Thibaut Courtois katika msimu uliopita na kujiunga rasmi na Arsenal hapo jumatatu.

Mourinho ameeleza kuwa alipendelea kuona nyota huyo anabaki kwenye kikosi hicho katika msimu huu lakini kwakuwa kwa sasa si chaguo namba moja katika kikosi cha timu hiyo lakini pia yeye mwenyewe kutaka kuondoka katika timu hiyo anamuungamkono mchezaji huyo na kuheshimu maamuzi yake.

Zaidi pia amemshukuru Cech kwakuwa sehemu ya mafanikio ya klabu hiyo,

“Petr amekuwa na msaada mkubwa kuitumikia Chelsea kwa miaka 11 na kushinda karibu kila kitu, daima nimekuwa nikihitaji kuona anabaki kikosini lakini naelewa yeye mwenyewe amekuwa akihitaji kuondoka hivyo naheshimu maamuzi yake”

Alisema Mourinho wakati anazungumza na tovuti ya klabu hiyo

Comments are closed.