MPANGO WA CHANJO YA HOMA YA UTI WA MGONGO WAFANIKIWA AFRIKA

MPANGO WA CHANJO YA HOMA YA UTI WA MGONGO WAFANIKIWA AFRIKA

Like
266
0
Wednesday, 11 November 2015
Global News

WATAALAMU wa Afya wamesema kuwa mpango wa chanjo kwa umma dhidi ya homa ya uti wa mgongo barani Afrika umepata mafanikio makubwa.

Zaidi ya watu milioni mbili walipata kinga dhidi ya maradhi hayo katika nchi 16 barani Afrika, ikiwemo Gambia na Ethiopia.

Shirika la Afya Duniani limesema katika kipindi cha mwaka 2013 kulikuwa na wagonjwa wanne wa Uti wa mgongo barani Afrika ingawa awali iliweka rekodi ya kuwa na maelfu ya vifo vinavyotokana na ugonjwa huo kila mwaka.

Comments are closed.