MPIGANAJI WA MWISHO WA TALIBAN AUAWA KANDAHAR

MPIGANAJI WA MWISHO WA TALIBAN AUAWA KANDAHAR

Like
287
0
Thursday, 10 December 2015
Global News

MPIGANAJI wa mwisho kati ya wapiganaji 11 wa Taliban ambao waliuzingira uwanja wa ndege wa Kandahar, Afghanistan ameuawa, zaidi ya saa 24, baada ya shambulizi kuanzishwa.

 

Wizara ya Ulinzi ya Afghanistan imesema leo kuwa watu 50 wakiwemo raia na maafisa wa usalama, wameuawa.

 

Shambulizi hilo ambalo ni kubwa dhidi ya kambi ya jeshi la anga nchini humo, lilifanyika sambamba na mkutano wa kikanda nchini Pakistan, ambako Rais Ashraf Ghani wa Afghanistan aliitaka Pakistan kusaidia kuanzisha tena mazungumzo ya amani na Taliban, yaliyovunjika mwanzoni mwa mwaka huu.

 

Comments are closed.