MRADI WA KUCHAKATA TAKA KUJENGWA KINONDONI

MRADI WA KUCHAKATA TAKA KUJENGWA KINONDONI

Like
316
0
Wednesday, 27 January 2016
Local News

HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni inatarajia kujenga mradi wa kuchakata taka hususani zile zinazozalishwa kwenye masoko yanayopatikana kwenye manispaa hiyo lengo ikiwa ni kuondoa taka hizo ili manispaa iwe safi.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar Es Salaam leo Meya wa Manispaa ya kinondoni Boniface Jacob amesema kuwa mradi huo unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 2 za kitanzania utajengwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Ujerumani, Halmashauri ya Hambag na Halmashauri ya Manispaa ya kinondoni.

Boniface ameeleza kuwa kutokana na manispaa ya kinondoni kuongoza kwa kuzalisha taka nyingi kutoka kwenye masoko, mradi huo utasaidia kuondoa kiasi kikubwa cha taka hizo kwa manufaa.

Comments are closed.