MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA TABORA-KOGA-MPANDA KUANZA HIVI KARIBUNI

MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA TABORA-KOGA-MPANDA KUANZA HIVI KARIBUNI

Like
463
0
Monday, 04 April 2016
Local News

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali ipo katika hatua za mwisho kuanza mradi wa ujenzi wa barabara ya Tabora-Koga-Mpanda yenye urefu wa Km. 356 kwa kiwango cha lami ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Awamu ya Tano aliyoitoa kwa wananchi wa Mikoa ya Katavi na Tabora.

 

Ametoa kauli hiyo wilayani Sikonge mkoani Tabora, mara baada ya kukagua barabara hiyo ambapo pamoja na mambo mengine amesema ujenzi huo unatarajia kuanza rasmi hivi karibuni.

 

Amesisitiza kuwa wananchi wanaostahili kulipwa fidia watalipwa kwa wakati kwa kuwa takribani shilingi bilioni moja zimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo.

Comments are closed.