MSAMA PROMOTIONS KUFANYA TAMASHA LA AMANI OCTOBER

MSAMA PROMOTIONS KUFANYA TAMASHA LA AMANI OCTOBER

Like
286
0
Wednesday, 23 September 2015
Local News

MSAMA promotions wanatarajia kufanya tamasha la amani October mwaka huu lenye lengo la kuhamasisha na kudumisha  amani kwa watanzania hususani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi na baada ya uchaguzi.

Mratibu wa Msama Promotion HUDSON KAMOGA ameiambia EFM  kuwa tamasha hilo litafanyika ndani ya mikoa kumi na kumalizika kabla ya uchaguzi huku akisisitiza kuwa watanzania wanatakiwa kuilinda amani na kuhakikisha nchi haiingii kwenye machafuko kutokana na siasa.

Comments are closed.