MSD KUFUNGUA DUKA KUBWA LA KISASA MUHIMBILI KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS

MSD KUFUNGUA DUKA KUBWA LA KISASA MUHIMBILI KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS

Like
288
0
Friday, 27 November 2015
Local News

SIKU chache baada ya Rais Dokta John Magufuli kuiagiza bohari ya dawa nchini-Msd-kufungua maduka ya dawa kwenye Hospitali za kanda na Taifa,  tayari agizo hilo limeanza kufanyiwa kazi ambapo bohari hiyo wiki ijayo inatarajia kufungua duka kubwa la kisasa ndani ya hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Mkurugenzi wa MSD, Laurean Bwanakunu amesema tayari maandalizi ya kufungua duka hilo yamekamilika nalinatarajia kufunguliwa wiki ijayo huku akibainisha kuwa litatumia mfumo maalum wa kielektroniki ili kuhakikisha dhima ya kuwezesha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba vyenye ubora kwa bei nafuu na kwa watanzania wote inatekelezwa kwa vitendo.

Comments are closed.