SHIRIKA la Madaktari wasio na Mipaka-MSF limesema kuwa wanatarajia kufanya majaribio juu ya aina tatu za dawa zinazoweza kutibu maradhi ya Ebola Mwezi Desemba katika vituo vya shirika hilo nchini Guinea na Liberia.
Majaribio mengine tofauti na hayo kuhusu aina mbili ya dawa, moja kutoka kampuni ya Chimerix ya Marekani na nyingine iliyotengenezwa na kampuni ya Fujifilm ya Japan yanalenga kutathmini namna Maji ya Damu ya wagonjwa waliopona Ebola yanavyoweza kusaidia kuwatibu watu walio na maradhi hayo.
Tangazo la MSF limesema matokeo ya mwanzo ya majaribio hayo yanaweza kuwa tayari mwezi Februari mwaka ujao.