Mstahiki Meya Wa Manispaa Ya Ubungo, Mhe Boniface Jacob, Aelezea Mipango wa Kuwawezesha, Wananchi wa Manispaa Ya Ubungo

Mstahiki Meya Wa Manispaa Ya Ubungo, Mhe Boniface Jacob, Aelezea Mipango wa Kuwawezesha, Wananchi wa Manispaa Ya Ubungo

Like
772
0
Tuesday, 22 May 2018
Local News

Meya wa Manispaa ya Ubungo, Mhe Boniface Jacob kwenye kipindi cha Joto la Asubuhi kinachorushwa kila siku kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia Saaa 12 hadi saa 3 Asubuhi leo tarehe 22,Mei, 2018 amefafanua kwa kina Miradi ya maendelea iliyoanzishwa, katika Manispaa yake.

Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na mradi wa maendeleo kwa Wanawake na Vijana ambapo alisema mradi huo unaendelea vizuri hivyo amewataka vijana ambao ni wakazi wa Manispaa hiyo wajitokeze kuomba mikopo kwa sababu hadi sasa idadi ya waliojitokeza kuomba mikopo ni ndogo.

“Kinachotakiwa ni kwamba waombaji wote watoke ndani ya Manispaa ya Ubungo hivyo vikundi vinatakiwa kufika kwenye Ofisi ya Mkurugenzi na utambulisho kweli wanaishi ndani ya manispaa hiyo, na waandae plan wanachokitaka kufanya kwa ajili ya mkoo wanaotaka.

Kama wanashindwa kuandaa hiyo plan kwa kukosa fedha za kuwapa watu wa kuandaa basi wafike tu kwenye ofisi yeyote ya kata, tumeweka wataalamu wetu ambao wameshaandaa muundo(Template) ya plan  wao watachukua na kubadilisha baadhi ya vitu kama vile jina la kikundi, majina ya waombaji na vingine”. Alisema Mhe. Jacob.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *