Watu takriban 20 wamefariki dunia na wengine wengi kujeruhiwa baada ya mti mkubwa kuwaangukia wakiogelea katika maporomoko ya maji eneo la Kintampo, Ghana.
Maporomoko hayo ni maarufu sana kwa watalii.
Watu hao walikuwa wakiogelea pale upepo mkubwa ulipoangusha mti na kusababisha mkasa huo, maafisa wa huduma za dharura wamesema.
Msemaji wa taifa wa huduma za dharura Prince Billy Anaglate alisema kisa hicho kilitokea katika maporomoko ya Kintampo, katika jimbo la Brong-Ahafo.
Kikosi cha pamoja na polisi na wahudumu za dharura kilifika eneo la mkasa kuwaokoa waliokwama chini ya mti huo.
“Mti mkubwa ulianguka mvua kubwa iliyoandamana na upepo ilipokuwa inanyesha na kuwaangukia watu hao,” aliyeshuhudia aliambia Starr News ya Ghana.
“WEngi walikuwa wanafunzi wa shule ya upili ya Wenchi Senior High. Wengine ni watalii. Tunajaribu kuwaokoa waliokwama chini ya mti huo kwa kuukata mti huo na matawi yake kwa msumeno.”
Bw Anaglate aliambia AFP kwamba wanafunzi 18 walifariki papo hapo na wengine wawili wakafariki wakitibiwa hospitalini.
ALisema watu 11 kwa sasa wanapokea matibabu, akiwemo mmoja wa maafisa wa shule hiyo aliyekuwa anasimamia ziara hiyo ya wanafunzi.
Taarifa nyingine zinasema waliojeruhiwa ni zaidi ya 20.
Wanatibiwa katika hospitali ya manispaa ya Kintampo.
“Tunatuma salamu za rambirambi kwa familia za waliofariki na kuwaombea waliojeruhiwa,” waziri wa utalii wa Ghana Catherine Abelema Afeku alisema kupitia