MTOTO WA GADDAFI AHUKUMIWA KUNYONGWA

MTOTO WA GADDAFI AHUKUMIWA KUNYONGWA

Like
302
0
Tuesday, 28 July 2015
Global News

MAHAKAMA moja nchini Libya imemuhukumu kuyongwa mtoto wa aliyekuwa Rais wa Taifa hilo Gaddafi, Saif al Islam na wengine nane kufuatia uhalifu wa kivita uliohusishwa na mapinduzi ya mwaka 2011.

Watuhumiwa hao walikuwa wameshitakiwa pamoja na washirika wengine wa kiongozi huyo aliyeondolewa madarakani kwa kujaribu kuzima maandamano wakati wa mapinduzi hayo.

Saif al Islam hakuwepo mahakamani na alitoa ushahidi wake kupitia teknolojia ya kanda ya video ambapo hadi sasa Saif anazuiliwa na kundi moja la waasi la zamani katika mji wa Zintan.

LIBYA2

Mahakama ya libya

 

 

Comments are closed.