MTOTO mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi na moja aliye tambulika kwa jina la Waziri Kashinje amefariki dunia baada ya kutumbukia katika shimo la maji wakati akicheza na wenzake katika nyumba ya jirani yao eneo la igoma Jijini Mwanza.
Akizungumza na E Fm katika eneo la tukio mjumbe wa serikali ya mtaa huo Amosi Shirangi amesema tukio hilo limetokea wakati mtoto huyo alipokuwa akicheza na wenzake lililopo katika nyumba ya jirani.
Nao Wazazi wa mtoto huyo Kashinje Kudema na mama wa mtoto huyo Bi. Sabina Eleniko wameelezea tukio hilo na kueleza kuwa wakati linatokea hawakuwepo eneo la tukio na walipatiwa taarifa hiyo na jirani aliye shuhudia mwili wa mtoto huyo ukielea juu ya maji.