MTU MMOJA ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUKAMATWA AKIVUNJA VIOO VYA GARI

MTU MMOJA ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUKAMATWA AKIVUNJA VIOO VYA GARI

Like
442
0
Tuesday, 24 February 2015
Local News

MTU mmoja Mkazi wa Dar e salaam, ambaye hujishughulisha na uokotaji wa makopo ya plastiki amenusurika kifo kutokana na  kipigo cha wananchi  baada ya kuvunja vioo vya nyuma vya magari  mawili ya wafanyakazi wa  bima ya AAR yaliyokuwa yameegeshwa nje ya ofisi hizo.

Kijana huyo aliyekuwa na jeraha  upande wa nyuma wa kichwa chake kikivuja Damu nyingi amejitambulisha  kwa jina Amir Ismail na kuiambia EFM  kuwa  kuna vijana sita wamemvamia na kumpora fedha zake shilingi elf 60 alizokuwa nazo.

Ismail ameeleza kuwa baada ya kuporwa pesa zake ndipo aliamua kuokota mawe na kupiga vioo vya magari hayo, kitendo kilichowakasirisha watu hao na kuanza kumpiga.

20150224_092003 20150224_092228 20150224_092653

Comments are closed.