MTUHUMIWA KATIKA SHABULIZI LA SEPT 11 AHUKUMIWA MAREKANI

MTUHUMIWA KATIKA SHABULIZI LA SEPT 11 AHUKUMIWA MAREKANI

Like
271
0
Friday, 27 February 2015
Global News

MAHAKAMA moja ya jijini New York, Marekani imemhukumu Khalid al-Fawwaz kwa kuhusika na mashambulizi ya mabomu ya balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania mwaka 1998.

Waendesha mashtaka wamemtaja al-Fawwaz kuwa mmoja wa watu waliokuwa karibu zaidi na aliyekuwa kiongozi wa al-Qaida, Osama bin Laden.

Baada ya mahakama kumkuta na hatia katika makosa 29, al-Fawwaz mwenye miaka 52 sasa anaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha. Raia huyo wa Saudi Arabia alikamatwa jijini London, Uingereza, mwaka 1998 na kukabidhiwa kwa Marekani mwaka 2012 baada ya mzozo wa kisheria uliochukua muda mrefu..

Comments are closed.