MUDA WAONGEZWA KUYAFIKIA MAKUBALIANO YA MPANGO WA NYUKLIA IRAN

MUDA WAONGEZWA KUYAFIKIA MAKUBALIANO YA MPANGO WA NYUKLIA IRAN

Like
219
0
Wednesday, 01 July 2015
Global News

IRAN na nchi zenye nguvu zaidi duniani zimeongeza muda wa kufikia makubaliano kamili kuhusu mpango wa kinyuklia wa Iran hadi tarehe saba mwezi huu baada ya kushindwa kufikia makubaliano hayo hapo jana.

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema baada ya miaka miwili ya mazungumzo kati ya nchi zinazohusika, anaamini makubaliano yako karibu yatafikiwa.

Rais wa Marekani Barack Obama hata hivyo amesisitiza nchi yake haitasita kujiondoa kutoka mazungumzo hayo ya kinyuklia iwapo masharti yanayotakiwa kutimizwa hayatakuwa ya kuridhisha.

Comments are closed.