NIGERIA leo imemwapisha bwana Muhammadu Buhari kuwa rais mpya wa nchi hiyo ambako zaidi ya nchi 30 za Afrika zinawakilishwa na viongozi katika sherehe hizo.
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini anahudhuria pia sherehe hizo wakati Marekani inawakilishwa na waziri wake wa mambo ya nchi za nje John Kerry,Uingereza na waziri wake wa mambo ya nchi za nje Philipp Hammond na Laurent Fabius anaiwakilisha Ufaransa.
Licha ya matatizo yanayolikabili taifa hilo linalochimba mafuta kwa wingi zaidi barani Afrika,ushindi wa kihistoria wa Muhammadu Buhari na tukio la kwanza la aina yake la kukabidhiwa madaraka kwa njia za kidemokrasia ,vimezusha matumaini mema kwa nchi hiyo.
Waziri wa maswala ya kigeni wa Marekani akiwa Abuja
Kiongozi wa Ethiopia akiwasili Abuja
Wasanii wakiwatumbuiza wageni
Rais Buhari akikagua guaride la heshima
Familia ya rais Buhari