MADAKTARI Bingwa wa Upasuaji kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na timu ya Madaktari wanne kutoka nchini Hispania wameendesha zoezi la upasuaji wa masikio, pua, pamoja na upasuaji wa shingo na kichwa.
Akizungumzia kuhusu zoezi hilo Daktari Bingwa wa magonjwa ya masikio, Pua na koo Martin Mushi amesema katika upasuaji huo madaktari hao wanatumia teknolojia kubwa na ya kisasa zaidi ambapo pamoja na mambo mengine ujio wao utawawezesha madaktari wa Muhimbili kujifunza zaidi matumizi ya teknolojia mpya ya upasuaji.
Aidha amesema awali wagonjwa hao walikuwa wakipelekwa nje ya nchi kwa ajili ya upasuaji lakini kwa sasa wagonjwa wanaohitaji upasuaji wa kawaida wanapata huduma hiyo Muhimbili.