MUHONGO AWASILISHA HOJA YA MKATABA KATI YA IPTL NA TANESCO

MUHONGO AWASILISHA HOJA YA MKATABA KATI YA IPTL NA TANESCO

Like
254
0
Thursday, 27 November 2014
Local News

WAZIRI WA NISHATI na Madini Profesa SOSPITER MUHONGO amewasilisha hoja yenye maelezo juu ya mkataba uliowekwa kati ya kampuni ya –IPTL-na shirika la umeme nchini Tanesco ambapo amesema kuwa taarifa iliyotolewa na kamati  ya  hesabu za serikali na mashirika ya umma- PAC- haina ukweli wowote kwa kuwa fedha za –ESCROW– siyo fedha za umma.

Akiwasilisha hoja hiyo leo Bungeni mjini Dodoma Profesa MUHONGO amesema kuwa ingawa kiasi hicho cha fedha za –ESCROW- siyo za umma pia hakuna ukweli wowote juu ya Tanesco kufungua kesi dhidi ya benki ya Standard chaterd.

 Mbali na hayo Profesa MUHONGO ametoa ufafanuzi juu ya maelezo yaliyotolewa na kamati ya –PAC- jana katika aya ya -1- iliyoeleza kuwa -PAP-siyo mmiliki halali wa hisa 7 za MECHIMER katika –IPTL-.

 

Comments are closed.