MUSEVENI AENDELEA NA MAZUNGUMZO YA AMANI BURUNDI KWA SIKU YA PILI

MUSEVENI AENDELEA NA MAZUNGUMZO YA AMANI BURUNDI KWA SIKU YA PILI

Like
470
0
Wednesday, 15 July 2015
Global News

RAIS wa Uganda Yoweri Museveni leo ameingia siku yake ya pili ya mazungumzo ya amani nchini Burundi.

Ikiwa imebaki siku chache tu kufanyika kwa uchaguzi wa Rais, inaonekana kuna nafasi ndogo ya Rais Museveni kuweza kushawishi lolote kuhusiana na msimamo wa Serikali ya Burundi kuhusiana na uchaguzi wa Burundi.

Mara baada ya kuwasili nchini Burundi, rais Museveni amewakumbusha raia wa Burundi moja ya jambo baya lililowahi kutokea nchini humo na ambalo halipaswi kuwepo kwa sasa ambalo ni mgawanyiko wa kikabila kati ya Wahutu na Watusi, na jambo la pili ni kudhani kuwa madarakani ndilo jambo la mhimu kuliko mambo mengine yote yanayoweza kuleta ustawi wa taifa zima.

Comments are closed.