RAIS wa Uganda Yoweri Museveni amesema ana imani atashinda urais kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika siku ya Alhamisi wiki hii.
Hata hivyo, amesema yuko tayari kukabidhi madaraka kwa mtu mwingine iwapo chama chake kitashindwa.
Akijibu maswali ya waandishi wa Habari wakati wa kikao kilichofanyika Ikulu jana Jumapili, Bwana Museveni amesema kwa sasa haoni chama chochote ambacho kinaweza kuondoa chama cha National Resistance Movement (NRM) madarakani.