MUSEVENI: WANAOKOSOA UCHAGUZI HAWAIJUI UGANDA

MUSEVENI: WANAOKOSOA UCHAGUZI HAWAIJUI UGANDA

Like
216
0
Monday, 22 February 2016
Global News

RAIS wa Uganda Yoweri Museveni amesema uchaguzi uliofanyika nchini humo Alhamisi wiki iliyopita ulikuwa wa haki na akasema wanaoutilia shaka hawaielewi Uganda.

 

Aidha, ametetea hatua ya maafisa wa usalama kumzuilia mgombea mkuu wa upinzani Dkt Kizza Besigye wa chama cha FDC.

 

Tume ya Uchaguzi ilisema Jumapili kwamba Bwana Museveni alipata ushindi wa asilimia 60.75 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Dkt Besigye aliyepata asilimia 37.35, lakini upinzani umedai kuwepo wizi wa kura na waangalizi wa kimataifa wamesema pia kwamba hakukuwa na nafasi sawa ya ushindani.

Comments are closed.