MUSWAADA WA SHERIA YA KUUNDWA KWA BARAZA LA VIJANA UMEHITIMISHWA LEO BUNGENI

MUSWAADA WA SHERIA YA KUUNDWA KWA BARAZA LA VIJANA UMEHITIMISHWA LEO BUNGENI

Like
326
0
Tuesday, 31 March 2015
Local News

MJADALA kuhusu Muswaada wa Sheria ya Kuundwa kwa Baraza la Vijana Tanzania umehitimishwa leo Bungeni Mjini Dodoma, ambapo Waziri na Naibu Waziri wenye dhamana ya Vijana wamepata nafasi ya kupitia hoja mbalimbali zilizotolewa na Wabunge juu ya kuundwa kwa Mabaraza hayo.

Akizungumza Bungeni Mjini  Dodoma  Waziri wa Habari,Utamaduni Vijana na Michezo Dokta FENELA MUKANGALA amesema Muswaada huo umekuwa halali baada ya kua umefuata taratibu sahihi tangu hatua ya awali ya kufanyiwa  matayarisho hadi kufikia hatua ya kupelekwa Bungeni.

Amebainisha kuwa Muswaada huo umeandaliwa baada ya kupata uzoefu kutoka nchi nyingine na sio mchezo wa Kukopi na Kupesti kutoka Kenya kama wasemavyo baadhi ya Wabunge.

Comments are closed.