MUUAJI WA ORLANDO ALITEMBELEA KLABU YA WAPENZI WA JINSIA MOJA

MUUAJI WA ORLANDO ALITEMBELEA KLABU YA WAPENZI WA JINSIA MOJA

Like
317
0
Tuesday, 14 June 2016
Global News

Ripoti kutoka Orlando Marekani zasema Omar Mateen, mtu aliyewafyatulia risasi na kuwaua watu 49 katika klabu moja ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, alikuwa akitembelea klabu hiyo iitwayo Pulse mara kwa mara.

Wahudumu na meneja wa klabu hiyo amenukuliwa na magazeti ya Marekani akisema kuwa, ameshawahi kumuona Mateen, hata akinywa pombe katika eneo hilo.

Naye mkewe wa zamani Sitora Yusufiy, amemwelezea Mateen kama mtu aliyekuwa na tabia za ugomvi wa mara kwa mara na kutaka kupigana na watu na wala hakuwa na itikadi kali za kidini.

Mke huyo pia anaongeza kusema kuwa, wakati mwengine alionekana kutokuwa na akili timamu.

Baadhi ya wateja wa klabu hiyo wanasema kwamba, alikuwa katika mtandao wa watu wa wapenzi wa jinsia moja.

Waandishi wa habari nao wanasema kuwa, taarifa zinazofichua alivyokuwa Mateen, zinaibua maswali chungu nzima kuhusiana na kiini cha shambulizi hilo, ambapo mshambuliaji anadi kuwa mfuasi wa kundi la kigaidi la Islamic State.

Maelfu ya watu walikesha usiku kucha kuwakumbuka watu hao 49 waliuawa.

Comments are closed.