MVUA YAUA 35 SHINYANGA

MVUA YAUA 35 SHINYANGA

Like
652
0
Wednesday, 04 March 2015
Local News

WATU 35 wamefariki dunia na wengine 55 kujeruhiwa baada ya nyumba zao kuwaangukia na kuwafunika usiku wa kuamkia leo kutokana na mvua kubwa iliyonyesha wilayani Kahama, mkoani Shinyanga.

Taarifa zilizothibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama,  Benson Mpesya amesema mvua hiyo kubwa iliambatana na upepo mkali, hivyo nyumba nyingi zilianguka na nyingine kuezuliwa na kuharibiwa kabisa. Mpesya amesema mpaka sasa wamefanikiwa kupata miili ya watu 35 waliopoteza maisha baada ya kufukua nyumba nyingi, na majeruhi wamekimbizwa hospitali ya wilaya kwa matibabu.

 

Comments are closed.