MWANAHABARI WA AL-SHABAAB AUAWA SOMALIA

MWANAHABARI WA AL-SHABAAB AUAWA SOMALIA

Like
558
0
Monday, 11 April 2016
Global News

MWANAHABARI aliyesaidia kundi la al-Shabaab kuua wanahabari wenzake nchini Somalia ameuawa.

 

Hassan Hanafi ameuawa kwa kupigwa risasi mapema asubuhi ya leo baada ya kuhukumiwa kifo na mahakama ya kijeshi nchini humo.

 

Hassan Hanafi, alipatikana na hatia ya kuwaua Sheikh Noor Mohamed Abkey (mhariri wa shirika la habari la SONNA), Sa’id Tahlil Warsame (mkurugenzi wa HornAfrik), na Mukhtar Mohamed Hirabe (mkurugenzi wa Radio Shabelle), na wanahabari wengine kadha.

Comments are closed.