MWANAHARAKATI APIGWA RISASI BURUNDI

MWANAHARAKATI APIGWA RISASI BURUNDI

Like
196
0
Tuesday, 04 August 2015
Global News

MWANAHARAKATI maarufu wa haki za kibinaadamu nchini Burundi amepigwa risasi na kujeruhiwa vibaya na watu waliokuwa katika pikipiki.

Pierre Claver Mbonimpa alishambuliwa katika mji mkuu wa Burundi Bujumbura ambapo pia kwa kipindi kirefu amekuwa mkosoaji mkubwa wa mchakato wa rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.

Siku ya jumapili mshauri wa rais huyo jenerali Adolphe Nshimirimana aliuawa katika shambulizi ndani ya gari lake Mjini Bujumbura wakati akisimamia usalama wa rais.

 

Comments are closed.