MWANAMKE ATOLEWA AKIWA HAI KWENYE KIFUSI NAIROBI

MWANAMKE ATOLEWA AKIWA HAI KWENYE KIFUSI NAIROBI

Like
275
0
Thursday, 05 May 2016
Global News

IMEBAINIKA kwamba Mwanamke amepatikana akiwa hai kwenye vifusi ikiwa ni siku sita baada ya jengo kuporomoka katika mtaa wa Huruma jijini Nairobi.

Kwa mujibu wa Pius Masai, mkuu wa kitengo cha taifa cha kukabiliana na majanga, amesema kuwa maafisa wa uokoaji bado wanajaribu kutengeneza njia ya kumtoa kwenye vifusi hivyo.

Hata hivyo, mwanamke huyo amekuwa akiwasiliana na matabibu ambao wanasubiri kumpatia matibabu punde atakapotolewa.

Comments are closed.