MWANASHERIA WA NELLY APANGA KUMNUSURU NA KESI YA DAWA ZA KULEVYA

MWANASHERIA WA NELLY APANGA KUMNUSURU NA KESI YA DAWA ZA KULEVYA

Like
354
0
Monday, 13 April 2015
Entertanment

Mwanasheria wa mkali wa ngoma zilizowahi kufanya vizuri ikiwemo Just a dream na Dilema ameanza kufanya harakati za utetezi kwa msanii huyo kwakudai dawa za kulevya alizokamatwa nazo hazikuwa zake.

Nelly alitiwa nguvuni na vyombo vya usimamizi wa sheria baada ya gari lake la msafara wa kikazi kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi na silaha ndani yake.

Mwanasheria huyo wa Nelly Scott Rosenblum kwenye mahojiano yake na mtandao wa Tmz amedai kuwa kulikuwa na zaidi ya watu 15 hadi 20 kwenye basi ambalo kila mtu alikuwa na nafasi ya kufanya anachojisikia hivyo Nelly hapaswi kuhusishwa na tuhuma hizo.

Comments are closed.