SERIKALI mkoani Mwanza imesema hakuna kulala hadi mtoto mwenye Ulemavu wa Ngozi PENDO EMMANUEL apatikane baada ya kutekwa na watu wasiojulikana.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza MAGESA MULONGO alipokuwa akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Ndami Wilayani Kwimba katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo.