MWANZA: MTOTO MWENYE ULEMAVU WA NGOZI APOTEA

MWANZA: MTOTO MWENYE ULEMAVU WA NGOZI APOTEA

Like
421
0
Friday, 02 January 2015
Local News

LICHA ya Serikali kufanya juhudi mbalimbali kukabiliana na Unyanyasaji wa Watu wenye Ulemavu wa ngozi-ALBINO nchini tatizo hilo limeendelea kujitokeza na kutishia amani yao.

Hali hiyo imejitokeza jijini Mwanza baada ya mtoto mwenye Ulemavu wa Ngozi PENDO SHIBINDE kutekwa nyumbani kwao katika kijiji cha Ndabi Wilaya ya Kwimba jijini Mwanza.

Akithibitisha kupotea kwa mtoto huyo Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza VALENTINO MLOWOLA amesema kila mtu anajukumu la kumlinda mtoto na kuachana na imani potofu ambazo zinapelekea watoto hao kudhuriwa, kupotea au kuuwawa.

Comments are closed.