MWANZA: TAHADHARI YATOLEWA KUFUATIA MLIPUKO WA HOMA YA NGURUWE

MWANZA: TAHADHARI YATOLEWA KUFUATIA MLIPUKO WA HOMA YA NGURUWE

Like
284
0
Friday, 11 December 2015
Local News

KUFUATIA kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa wa Homa ya Nguruwe MKoani Mwanza, wafugaji wametakiwa kuepuka kununua Nguruwe kutoka kwenye Maeneo au Mashamba yenye ugonjwa Nguruwe na kutakiwa wafugwe kwenye Mabanda imara ili waepuke kutembea ovyo , Nguruwe wasilishwe mizoga au masalio ya chakula kutoka vyanzo visivyojulikana .

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Dokta Yohana Sagenge , Mlipuko huo umedhibitishwa kutokana na uchunguzi uliofanyawa na Maabara ya Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) nakubainishwa kuwa Ugonjwa wa Homa ya Nguruwe unasababishwa na Virusi.

Comments are closed.