MWENGE WA UHURU WAKABIDHIWA KWA MKUU WA WILAYA YA KINDONDONI

MWENGE WA UHURU WAKABIDHIWA KWA MKUU WA WILAYA YA KINDONDONI

Like
267
0
Friday, 29 May 2015
Local News

MWENGE  wa uhuru umekabidhiwa leo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda baada ya hapo jana kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya ya Ilala yenye gharama ya  shilingi bilioni 14.

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa miradi hiyo jana, Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru,  Juma Chumu  amewataka Watanzania  kutunza miradi mbalimbali ya mandeleo inayoletwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau na wananchi wenyewe.

 

Amesema kuwa mbio za mwenge mwaka huu zinatumika katika kutoa elimu na kuhimiza watanzania kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili kuweza kuchagua viongozi wanaofaa  na kuleta mabadiliko kwa Taifa. Mwenge huo pia unatarajiwa kuzindua miradi mbalimbali katika Wilaya ya Kinondoni.

 

Comments are closed.