MWENYEKITI wa chama cha walimu nchini (CWT) Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Abraham Kisimbi amesema atawatetea walimu wa wilaya hiyo ambao wanadai serikalini fedha zao ikiwemo kurudishiwa asilimia 15 ya fedha zao.
Akizungumza baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo, Kisimbi ameeleza kuwa walimu wa wilaya hiyo wana changamoto kubwa ikiwemo kutopandishwa daraja kwa muda mrefu, hivyo amesema atatumia nafasi hiyo kutetea haki zao.