MWENYEKITI WA TAASISI YA WAMA AKABIDHI MASHINE ZA UPIMAJI WA SARATANI YA MATITI

MWENYEKITI WA TAASISI YA WAMA AKABIDHI MASHINE ZA UPIMAJI WA SARATANI YA MATITI

Like
308
0
Friday, 27 February 2015
Local News

MWENYEKITI  wa Taasisi ya Wanawake Tanzania-WAMA amekabidhi msaada wa mashine ya kisasa ya upimaji Saratani ya Matiti  kwa akinamama katika hospitali kuu ya Jeshi la Ulinzi Tanzania LUGALO ili kuokoa  maisha ya wanawake wengi wanaosumbuliwa na Saratani ya matiti nchini.

Akizungumza na wadau mbalimbali leo Jijini Dar es Salaam kwenye makabidhiano ya mashine hiyo  Mama SALMA KIKWETE ambaye pia ni mke wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameeleza kuwa mashine imetolewa na kikundi cha wanawake watanzania waishio Marekani kijulikanacho kama Tano Ladies lengo likiwa ni kupanua wigo wa utoaji huduma za saratani kwa wananchi waliyo wengi hususani wanawake.

Amebainisha kuwa ameamua kukabidhi mashine hiyo katika hospitali ya Jeshi Lugalo kwa kuwa idadi kubwa ya wanawake hupendelea zaidi kupata huduma za kiafya kwenye hospitali hiyo lakini pia ni kituo cha kutolea huduma kwa wanawake na watoto.

 

Comments are closed.