MWILI WA AISHA MADINDA KUZIKWA LEO

MWILI WA AISHA MADINDA KUZIKWA LEO

Like
327
0
Friday, 19 December 2014
Local News

 

MWILI wa aliyekuwa mnenguaji wa bendi za Twanga Pepeta na Extra Bongo, Aisha Mohamed Mbegu maarufu Aisha Madinda unazikwa leo nyumbani kwao Kigamboni Jijini Dar es salaam.

 Mazishi hayo yalitarajiwa kufanyika jana, lakini yalilazimika kuahirishwa baada ya Jeshi la polisi kuzuia hadi hapo mwili wake utakapofanyiwa uchunguzi kutokana na utata wa kifo chake.

 Awali akizungumza na Efm, Mkurugenzi wa Asset, inayomiliki bendi ya Twanga pepeta, Asha Baraka amewataka watu wote kumwombea Marehemu Aisha ili mwenyezi mungu amlaze mahali pema peponi.

Comments are closed.