MWILI WA CELINA KOMBANI KUWASILI NCHINI JUMATATU

MWILI WA CELINA KOMBANI KUWASILI NCHINI JUMATATU

Like
261
0
Friday, 25 September 2015
Local News

MWILI wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Ompeashi Kombani unatarajiwa kuwasili nchini siku ya Jumatatu.

 

Taarifa kutoka ofisi za Bunge ambazo zilithibitisha kifo hicho zimeeleza kuwa Bunge na Serikali watasimamia maandalizi yote ya maziko na kumsafirisha kwa mazishi nyumbani kwa marehemu huko Mahenge ambako alikuwa Mbunge wa jimbo la Ulanga Mashariki.

 

Mheshimiwa  Kombani amefariki dunia jana huko India alikokuwa akipata matibabu ya saratani. Alikuwa na umri wa miaka 56.

Comments are closed.