MWONGOZO WA KUANDAA BAJETI WAWASILISHWA BUNGENI LEO

MWONGOZO WA KUANDAA BAJETI WAWASILISHWA BUNGENI LEO

Like
345
0
Monday, 01 February 2016
Local News

WIZARA ya Fedha na Mipango leo imewasilisha mapendekezo ya Mpango wa maendeleo ya Taifa pamoja na mwongozo wa kuandaa mpango na bajeti ya serikali ya mwaka 2016/2017 unaolenga utekelezwaji wa vipaumbele mbalimbali vya kuleta maendeleo.

Akiwasilisha mapendekezo ya mpango na mwongozo huo Bungeni Mjini Dodoma, Waziri wa Fedha na Mipango dokta Philip Mpango amesema kuwa mpango huo unalenga kuinua kwa kiasi kikubwa uchumi wa Taifa.

Awali mpango huo haukuweza kujadiliwa siku chache zilizopita kutokana na serikali kuuwasilisha kimakosa hali iliyosababisha kuwasilishwa tena leo.

Comments are closed.