KIONGOZI wa upinzani nchini Myanmar Aung Suu Kyi, leo ametoa wito wa kuwepo kwa mazungumzo ya kitaifa ya upatanishi kati ya rais wa Myanmar na mkuu wa jeshi la nchi hiyo lenye nguvu kubwa kisiasa baada ya chama chake kuonekana kupata ushindi wa kishindo katika Uchaguzi mkuu.
Chama cha National League for Demcracy-NLD-kimeonekana kupata madaraka baada ya kupata asilimia 90 ya viti vilivyotangazwa hadi sasa sawa na viti 163 kati ya viti 182 vilivyotangazwa hadi sasa.
Licha ya maafisa wa uchaguzi kutotangaza kwamba chama cha NLD kimeshinda, madaraka ya nchi hiyo yaliyokuwa mikononi mwa jeshi kwa nusu karne , yanaelekea kubadilika.