MZEE WA MIAKA 55 MABARONI KWA KUMBAKA MTOTO

MZEE WA MIAKA 55 MABARONI KWA KUMBAKA MTOTO

Like
221
0
Tuesday, 08 September 2015
Local News

JESHI la polisi mkoani Iringa lina mshikilia mtu mmoja anayefahamika kwa jila la Augustino kavindi mwenye umri wa miaka 55 makazi wa Tanangozi kwa tuhuma za kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka mitatu na kumsababishia maumivu makali mtoto huyo.

 

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani humo Ramadhan Mungi amesema kuwa kuwa kabla ya jeshi la polisi kumkamata mtuhumiwa huyo alinusurika kuuwawa na wananchi wenye hasira kali kwa kutokana na kitendo hicho.

 

Wakati huo huo mwili wa kijana aliyefahamika kwa jina la Robinus lingstoni kiando umekutwa umetelekezwa huku ukiwa na majeraha katika baadhi ya maeneo ya mwili wake.

Comments are closed.