WAZIRI wa Mambo ya nje wa Saudi Arabia amesema kuwa mzozo unaozidi kufukuta kati ya Riyadh na Tehran hautaathiri mazungumzo ya amani ya Syria.
Taarifa yake ilikuja wakati Kuwait nayo ikimrudisha balozi wake kutoka Iran, kuiunga mkono Saudi Arabia.
Saudi Arabia pamoja na mataifa mengine kadhaa ya Kiarabu, yamechukuwa hatua dhidi ya Iran, baada ya ubalozi wake kushambuliwa na kuchomwa moto na waandamanaji waliokuwa wanapinga kuuawa kwa kiongozi wa Kishia na mkosoaji wa serikali ya Saudi Sheikh Nimr al-Nimr.