MZOZO WAIBUKA KATI YA HUNGARY, UFARANSA

MZOZO WAIBUKA KATI YA HUNGARY, UFARANSA

Like
174
0
Monday, 31 August 2015
Global News

MZOZO wa kidiplomasia umeibuka kati ya Hungary na Ufaransa juu ya uamuzi wa Hungary kuweka ukuta katika mpaka wake na Serbia ili kuzuia kuingia wahamiaji haramu.

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius amesema kuwa ujenzi wa ukuta huo  ni ukiukaji wa maadili ya nchi za ulaya.

Hata hivyo mwenzaeke kutoka upande wa Hungary Peter Szijjarto ameelezea kushangazwa kwake na madai hayo nakusema kuwa bara la Ulaya linastahili kushirikiana kukabiliana na tatizo la uhamiaji haramu badala ya kuelekezeana lawama

Comments are closed.