NAIBU WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO AMESEMA SERIKALI HAINA NIA YA KUFUNGIA CHOMBO CHOCHOTE CHA HABARI

NAIBU WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO AMESEMA SERIKALI HAINA NIA YA KUFUNGIA CHOMBO CHOCHOTE CHA HABARI

Like
234
0
Thursday, 29 January 2015
Local News

SERIKALI kupitia Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe.Juma Nkamia imesema haina nia ya kufungia chombo chochote cha habari, lakini pia imesisitiza kuwa hakuna Uhuru usio na mipaka.

 

Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA, katika kipindi cha Maswali na majibu, aliyetaka kujua kwanini Serikali haioni haja ya kulifungulia gazeti la Mwanahalisi ili kutoa uhuru kwa wananchi kupata habari kwa wakati.

 

Mheshimiwa Nkamia amesema ili kujiepusha na matatizto kama hayo ni vyema wandishi wakazingatia maadili ya taaluma yao ya habari.

 

Bunge linaendelea na kikao chake cha tatu, mkutano wa 18, ambapo tayari limeanza kujadili hoja ya Dharula iliyowasilishwa jana na Mbunge wa Kuteuliwa James Mbatia kuhusu sakata la kukamatwa kwa Mwenyekiti wa chama cha wananchi-cuf, Profesa Ibrahim Lipumba.

Comments are closed.